MASHINE HATARI YATUA YANGA
Khadija Mngwai na Hans Mloli KUMEKUCHA Jangwani! Huenda ukawa ni
mwaka mwingine wa neema Yanga kutokana na kikosi hicho kusukwa vizuri
kwa ajili ya mashindano. Kwa taarifa ni kwamba yule straika msumbufu kwa
mabeki, Donald Ngoma, raia wa Zimbabwe, anatarajiwa kutua Yanga wakati
wowote ndani ya wiki hii kwa ajili ya kumalizana na timu hiyo. Hayo yote
yamekuja baada ya TFF kupitisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni na
Yanga inataka kuitumia nafasi hiyo kujiboresha kwa ajili ya michuano ya
kimataifa na Ligi Kuu Bara msimu ujao. Tayari Ngoma ameshatumiwa tiketi
na sasa kinachosubiriwa ni kutua kwake tu. Inaelezwa kuwa Mwenyekiti wa
Yanga, Yusuf Manji, yupo tayari kumwaga fedha sasa kuhakikisha kikosi
chake kinakuwa bora kimataifa. Makubaliano ya awali ni kwamba Ngoma…
Post a Comment