Ralph R. Debbas, ni mkurugenzi wa kampuni mpya ya magari W Motors iliyopo Dubai.
Na baada ya ujio wao kwenye ulimwengu wa magari, kampuni hii imeanza
kutengeneza headlines za kipeke duniani, ikiwa ni kampuni ya kwanza ya
kiarabu kutengeneza magari yanayoipiku brand kubwa za magari duniani
kama Ferrari, Lambroghini na Buggati.
Toleo la kwanza la gari kutoka kwa W Motors ni supercar Lykan Hypersport,
gari lililotokea kuweka headlines kubwa kwenye mitandao ya kijamii kama
Instagram pamoja na internet na headlines zilizopo sasa hivi ni kwamba
gari hili laweza kuja kuwa gari la kifarhari kushinda yote duniani.
Nimekusogezea baadhi ya picha za gari hili hapa chini ila na wewe uweze kujionea.
Mwezi wa sita mwaka huu, Lykan Hypersport lilitangazwa kuwa gari la kwanza la kifahari kutumika na polisi wa Abu Dhabi
Gari hilo sasa hivi lipo kwenye ukaguzi kuona kama litafaa kwa shughuli za kipolisi.
W
Motors sasa hivi wako mezani na project nyingine ya gari hili litakalo
itwa SuperSport Car, yatakayo tengenezwa 25 tu kwa mwaka.
Post a Comment