Wiki moja baada ya ofa ya kwanza ya Manchester United kumsajili Sergio Ramos kukataliwa na Real Madrid, hatimaye mchezaji huyo ambaye yupo mapumzikoni ametoa kauli yake.
Hata hivyo baada ya Ramos kugundua Madrid wameikataa ofa hiyo, alichukua uamuzi wa kuwaweka wazi viongozi wa Madrid kupitia wakala wake kwamba – Anataka kuondoka na kujiunga na United na kuiomba Madrid ikubaliane bei na Manchester United.
Madrid wanategemewa kujaribu kumtuliza Ramos na mkataba mnono mpya lakini kaka na meneja wa mchezaji huyo – Rene Ramos ameshaifahamisha(hekahekazangu blogsport.com) Madrid lengo la mteja wake kutaka kuanza maisha mpya sehemu nyingine.
Rene ameripotiwa kusema kwamba Ramos anataka kuhamia Old Trafford wakati huu wa dirisha la usajili na klabu pekee ambayo anataka Madrid ifanye nayo makubaliano ni United.
Post a Comment